Kitengo cha utumishi kinasafisha maeneo yanayozunguka Atabatu Abbasiyya tukufu

Kitengo cha utumishi katika Atabatu Abbasiyya kinasafusha maeneo yote tanayozunguka malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s).

Makamo rais wa kitengo Sayyid Ahmadi Mahmudu amesema “Watumishi wetu wanasafisha maeneo yanayozunguka Atabatu Abbasiyya tukufu kama sehemu ya kujiandaa kupokea mwezu mtukufu wa Muharam”.

Akaongeza kuwa “Kazi hiyo inafanywa na idara ya usafi chini ya kitengo, inatumia mitambo maalum”, akasema “Sehemu zinazo safishwa ni pamoja na njia za mitaa na barabara zote zinazo elekea kwenye malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s)”.

Atabatu Abbasiyya tukufu inafanya kazi kubwa ya kusafisha maeneo yote ya karibu na malalo takatifu, kutokana na kukaribia mwezi mtukufu wa Muharam.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: