Mkuu wa tawi la Maahadi ya Qur’ani katika wilaya ya Hindiyya chini ya Majmaa Sayyid Haamid Mar’abiy amesema “Maahadi imehitimisha mradi wa semina za Qur’ani katika wilaya ya Hindiyya, kwa kufanya hafla ya usomaji wa Qur’ani ambapo watashiriki wanafunzi zaidi ya elfu 4 kutoka maeneo tofauti ya wilaya ya Hindiyya”.
Akaongeza kuwa “Zaidi ya walimu 125 wameshiriki katika ufundishaji wa semina hizo, miongoni mwa mada zilizofundishwa ni, Kuhifadhi, Usomaji, Fiqhi, Aqida, Sira na Akhlaq, semina zimedumu kwa muda wa siku 45, zimelenga kujenga utamaduni wa usomaji wa Qur’ani na maadili mema katika jamii”.
Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu hufanya semina hizi kila mwaka wakati wa likizo za majira ya kiangazi katika shule za sekula, kwa lengo la kutengeneza kizazi chema cha watu wanaopenda Qur’ani tukufu na mafundisho ya Dini tukufu ya kiislamu kwa mujibu wa muongozo wa Ahlulbait (a.s).