Atabatu Abbasiyya tukufu imewapa zawadi washiriki wa kongamano la kielimu awamu ya pili kuhusu fatwa tukufu ya kujilinda.
Kongamano limesimamiwa na Ataba tukufu chini ya uratibu wa kikosi cha Abbasi (a.s) kwa kushirikiana na chuo cha ulinzi wa taifa, limejikita katika kuangazia ulinzi wa umma na kupambana na changamoto za kifikra na kiusalama.
Waliopewa zawadi ni: Rais wa kamati ya elimu ya kongamano ambae ni mjumbe wa kamati kuu ya Ataba tukufu Dokta Abbasi Didah Mussawi, makamo katibu mkuu wa Ataba Sayyid Maitham Zaidi na rais wa kamati ya maandalizi ya kongamano Meja jenerali Dokta Ali Handuli Shimri.
Atabatu Abbasiyya inafanya kila iwezalo katika kuingiza swala hilo kwenye historia ya Iraq, kwa njia za kielimu na kitamaduni, ikiwemo kufanya makongamano ya kielimu, kufadhili tafiti za kisekula kwa lengo la kulinda kumbukumbu za taifa na misingi iliyopelekea kupatikana kwa fatwa takatifu ya kujilinda.