Kueneza mabango yanayoashiria huzuni kwenye eneo ya katikati ya haram mbili ikiwa ni sehemu ya kujiandaa kupokea mwezi mtukufu wa Muharam

Watumishi wa kitengo kinacho simamia uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu katika Atabatu Abbasiyya, wameweka mabango yanayoashiria huzuni ikiwa ni sehemu ya kujiandaa kuupokea mwezi mtukufu wa Muharam.

Uwekaji wa mabango hayo kwenye eneo la katikati ya haram mbili ni sehemu ya mkakati maalum wa kupokea msimu wa huzuni.

Vitengo vya Atabatu Abbasiyya tukufu hufanya kila viwezalo katika kuweka mazingira ya huzuni, aidha hujiandaa kutoa huduma mbalimbali kwa waombolezaji ambao huja kufanya ziara katika Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya ifikapo miezi ya huzuni kwa Ahlulbait (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: