Kitengo kinachosimamia haram kimekamilisha maandalizi ya kupokea mwezi wa Muharam

Kitengo kinachosimamia haram tukufu katika Atabatu Abbasiyya, kimekamilisha maandalizi ya kupokea mwezi wa Muharam.

Makamo rais wa kitengo Sayyid Zainul-Aabidina Quraish amesema “Watumishi wa kitengo wamekamilisha maandalizi ya kupokea mwezi mtukufu wa Muharam, kwa mujibu wa utaratibu uliowekwa na uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu”.

Akaongeza kuwa “Maandalizi yalianza kwa kutandua mazulia ndani ya haram tukufu, kisha ikatandikwa nailoni halafu juu yake zikatandikwa kapeti nyekundu kwenye eneo la ukubwa wa mita elfu 10, kwenye uwanja wa milango na ndani ya Ataba tukufu”, akasema kuwa “Kazi hiyo imefanywa kwa kushirikiana na vitengo vingine”.

Akafafanua kuwa “Maandalizi yanajumuisha kuandaa uwanja wa Ummul-Banina (a.s), ili uendelee kupokea mazuwaru ndani ya mwezi mtukufu wa Muharam”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: