Kwa picha.. shughuli ya kubadili bendera ya kubba la malalo ya Imamu Hussein (a.s) kama sehemu ya tangazo la kuingia mwezi wa Muharam

Imeshushwa bendera nyekundu kwenye kubba la malalo ya Imamu Hussein (a.s) siku ya Alkhamisi na kupandishwa bendera nyeusi ikiwa kama tangazo la kuingia mwezi wa Muharam.

Shughuli hiyo imefanywa mbele ya idadi kubwa ya mazuwaru, waliokuja Karbala kuhuisha usiku wa kwanza wa mwezi mtukufu wa Muharam kutoka ndani na nje ya Iraq.

Shughuli hiyo imehudhuriwa na kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Husseiniyya Muheshimiwa Shekhe Abdulmahadi Karbalai, ambae ameongea katika tukio hilo.

Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya zimeandaa utaratibu maalum wa kuendesha shughuli ya kubadili bendera za malalo ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) baada ya swala ya Magharibi na Isha.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: