Kazi ya kubadili bendera imefanywa na katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya Sayyid Mustwafa Murtadha Aalu Dhiyaau-Dini.
Wahudumu wa Ataba tukufu wameweka mabango na mapambo meusi kwenye minara na korido za haram tukufu pamoja na uzio wa nje.
Ubadilishaji wa bendera umefanywa kufuatia tangazo la ofisi ya Marjaa-Dini mkuu Ayatullahi Sayyid Husseini Sistani kuwa Ijumaa ya kesho ni siku ya kwanza ya mwezi wa Muharam (1447h).