Majlisi imefanywa wakati wa kubadili bendera ya kubba la malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), iliyoratibiwa na Atabatu Abbasiyya na kuhudhuriwa na kiongozi mkuu wa Ataba tukufu muheshimiwa Allamah Sayyid Ahmadi Swafi, viongozi wa kidini, hauza na kundi kubwa la mazuwaru.
Mzungumzaji alikuwa ni Shekhe Abduswahibu Twaiy, ameongea historia ya Imamu Hussein (a.s) na safari yake na watu wa nyumbani kwake ya kwenda Karbala, akafafanua athari ya safari hiyo katika kunusuru uadilifu na kuthibitisha haki sambamba na subira na kujitolea.
Majlisi ikahitimishwa kwa kusoma qaswida na mashairi kutoka kwa Muhammad Fatwimiy, yaliyoelezea tukio la Twafu na msiba waliopata Ahlulbait (a.s) katika siku ya Ashura.