Mhadhiri wa Majlisi Sayyid Hishaam Albatwatwa amesema “Majlisi imefanywa saa saba mchana ndani ya ukumbi wa malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), itadumu kwa muda wa siku kumi”, akaongeza kuwa “Wakati wa majlisi hautatizi kupita mawakibu Husseiniyya”.
Akaongeza kuwa “Majlisi zinamaudhui nyingi, miongoni mwake ni maudhui za kifikra, itikadi, maadili, malezi, historia, tukio la Ashura na Imamu Hussein (a.s), pamoja na mambo mengine mengi”.
Atabatu Abbasiyya tukufu huomboleza kumbukumbu ya Ashura na kubainisha dhulma aliyofanyiwa Imamu Hussein (a.s) na malengo ya harakati yake ya milele.