Idara ya wahadhiri wa Husseiniyya tawi la wanawake, chini ya ofisi ya kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya, imefanya majlisi ya kuomboleza kufuatia kuingia kwa mwezi mtukufu wa Muharam.
Majlisi imefunguliwa kwa Qur’ani tukufu, ikafuatiwa na ziara ya Ashura kisha muhadhara wenye anuani isemayo (Hussein “a.s” ni msingi wa nuru kwa kila mtu), imefafanua nafasi ya bwana wa mashahidi (a.s) mbele ya babu yake Mtume (s.a.w.w).
Majlisi ikahitimishwa kwa kusoma qaswida na tenzi za Husseiniyya zilizoeleza tukio la Twafu.
Idara ya wahadhiri wa Husseiniyya hufanya majlisi za kuomboleza kuanzia siku ya kwanza ya mwezi mtukufu wa Muharam hadi tarehe kumi na saba ya mwezi huo katika kituo cha Swidiqatu Twahirah (a.s), sambamba na kufanya majlisi hizo katika maeneo ya nje kupitia mradi wa (mawaidha mema).