Mawakibu Husseiniyya zimeanza kuomboleza mwezi wa Muharam 1447h

Barabara zinazoelekea kwenye malalo ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) zimeshuhudia makundi makubwa ya mawakibu Husseiniyya katika siku ya kwanza ya mwezi mtukufu wa Muharam mwaka 1447h.

Mawakibu za wenye zanjiil zimekuja kuomboleza kifo cha Imamu Hussein na watu wa nyumbani kwake (a.s), kupitia utaratibu wa uombolezaji ambao hufanywa kila mwaka katika mwezi wa Muharam.

Mawakibu zitaendelea kufanya matembezi mwezi mzima, chini ya utaratibu maalum ulioandaliwa na kitengo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya.

Mawakibu hutembea katika barabara maalum zinazoelekea kwenye malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), wakipita katika ukumbi mtukufu wa haram yake, halafu wanaingia kwenye uwanja wa katikati ya haram mbili na wanaenda hadi kwenye malalo ya bwana wa mashahidi Imamu Hussein (a.s).

Kitengo cha maadhimisho kimeteua kikosi maalum kinacho fuatana na kila maukibu kuanzia mwanzo hadi mwisho, kinasimamia mpangilio wa matembezi na kuzuwia msongamano, ili kuepusha kugongana kwa mawakibu au kuleta usumbufu kwa mazuwaru, kila maukibu inatumia barabara iliyopangiwa.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: