Kufuatia kuingia mwezi wa Muharam.. Atabatu Abbasiyya imefanya majlisi ya kuomboleza nchini Ujerumani

Atabatu Abbasiyya tukufu imefanya majlisi ya kuomboleza katika nchi ya Ujerumani, kufuatia kuingia kwa mwezi wa Muharam mwaka 1447h.

Muwakilishi wa Atabatu Abbasiyya barari Ulata Sayyid Ahmadi Radhwi amesema “Majlisi imefanywa katika mji wa Gottingen, kuomboleza kumbukumbu ya kifo cha Imamu Hussein (a.s) na itaendelea hadi mwezi kumi Muharam”.

Akaongeza kuwa “Ratiba ya majlisi imehusisha usomaji wa Qur’ani tukufu, ziara ya Sayyid Shuhadaa (a.s), kusoma tenzi na qaswida pamoja na kuswali jamaa”.

Raadhwi amesema kuwa “Majlisi inatoa mafundisho ya Dini kwa lugha ya Kijerumani”, akaongeza kuwa, “Muwakilishi wa Ataba tukufu amesemamia ugawaji wa chakula kwa washiriki”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: