Uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu unafanya majlisi za kuomboleza ndani ya ukumbi wa utawala kuhuisha mwezi mtukufu wa Muharam mwaka 1447h.
Majlisi imefunguliwa kwa Qur’ani tukufu, ikafuatiwa na muhadhara kutoka kwa Shekhe Haazim Atwani, ameongea historia ya Imamu Hussein (a.s) na safari yake hadi Karbala, sambamba na kufafanua athari ya kudumu ya safari hiyo, katika kunusuru haki na kuimarisha uadilifu, bila kusahau mafunzo ya subira na kujitolea.
Majlisi imehudhuriwa na kundi kubwa la wahudumu wa Ataba, viongozi wa Ataba na mazuwaru.
Muhadhara umejikita katika kueleza historia ya Abulfadhil Abbasi (a.s) na ushujaa wake.
Majlisi ikahitimishwa kwa kusoma tenzi na qaswida za Husseiniyya zilizo amsha hisia za huzuni na majonzi.
Atabatu Abbasiyya tukufu hufanya majlisi za Husseiniyya kwa lengo la kuhuisha utajo wa Ahlulbait (a.s) na kueleza historia na utukufu wao.