Idara ya wahadhiri na maelekezo ya kidini zinaendelea na kufanya majlisi za Husseiniyya ndani ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s).

Idara ya wahadhiri wa Husseiniyya tawi la wanawake na maelekezo ya kidini, chini ya ofisi ya kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya, zinafanya majlisi za Husseiniyya katika malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s).

Idara hizo zinafanya majlisi za kuomboleza katika Sardabu ya Imamu Mussa Alkadhim (a.s) ndani ya Atabatu Abbasiyya mbele ya kundi la mazuwaru wa malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), kutokana na umuhimu wa majlisi hizo zinazohamasisha kufuata mwenendo wa bwana wa mashahidi (a.s).

Majlisi za kuomboleza zitaendelea hadi mwezi kumi na tatu Muharam, zinahusisha usomaji wa Qur’ani tukufu, Ziaratu-Ashuraa pamoja na muhadhara wa kidini na igizo linalo onyesha tukio la Twafu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: