Majlisi imehudhuriwa na kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya, Muheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi, katibu mkuu Sayyid Mustwafa Murtadha Aalu Dhiyaau-Dini, viongozi wengine wa Ataba, wahudumu na kundi kubwa la mazuwaru na waombolezaji.
Majlisi imefunguliwa kwa Qur’ani tukufu, iliyofuatiwa na muhadhara kutoka kwa Shekhe Haazim Atwiwaani, amebainisha ulazima wa kuamrisha mema na kukataza mabaya, akasisitiza kuwa umma wa kiislamu hautakiwi kuacha jambo hilo, madam unafuata mwenendo wa Mtume Muhammad na watu wa nyumbani kwake (a.s).
Majlisi ikahitimishwa kwa kusoma tenzi na qaswida za Husseiniyya zilizo amsha hisia za huzuni na majonzi katika nyoyo za waumini.
Atabatu Abbasiyya hufanya majlisi za kuomboleza kifo cha Imamu Hussein na watu wa nyumba ya Mtume (a.s) kila mwaka.