Idara ya kutandika mazulia katika haram tukufu, imetandika mita za mraba 2080 za mazulia mekundu, kama sehemu ya mkakati maalum wa kupokea mazuwaru katika mwezi huu wa huzuni, na kutoa huduma bora kwa mawakibu na mazuwaru wa Husseiniyya.
Kazi ya kutandika mazulia imehusisha uwanja unaozunguka dirisha takatifu la Abulfadhil Abbasi (a.s) na korido zake zinazoelekea sehemu hiyo, aidha zulia zimeshikanishwa kwa gundi maalum ili kuweka uimara zaidi.