Makamo rais wa kitengo Sayyid Ali Mussa Imram amesema “Wahudumu wa kitengo wanafanya kazi kubwa ya kupoza hali ya hewa kwa kutumia mitambo ya viyoyozi ndani ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) na Sardabu yake, sambamba na kuweka maji baridi ya kunywa”.
Akaongeza kuwa “Kitengo kinafanya kazi ya kufunga viyoyozi katika uwanja wa Ummul-Banina (a.s) yenye uwezo wa tani 200, itakayo toa huduma kwa mazuwaru watukufu”.
Akabainisha kuwa “Wahudumu wetu pia wanasimamia kiwanda cha kutengeneza barafu kilicho chini ya Ataba tukufu, kwa ajili ya kutengeneza barafu na kuzigawa kwa mawakibu zinazoshiriki kwenye ziara ya Ashura”.