Atabatu Abbasiyya inaendelea kufanya majlisi za kuomboleza ndani ya ukumbi wa malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), katika siku ya sita ya mwezi mtukufu wa Muharam mwaka 1447h.
Majlisi ambazo hufaywa kumi na kwanza katika mwezi wa Muharam, husimamiwa na idara ya wahadhiri wa Husseiniyya katika Ataba tukufu, mbele ya viongozi wa Ataba na wahudumu, bila kusahau mazuwaru watukufu.
Majlisi imepambwa na muhadhara kutoka kwa Sayyid Hashim Batwatwa, ameongea kuhusu mafundisho yanayopatikana katika mapambano ya Imamu Hussein (a.s) na athari yake katika zama za sasa, akahimiza kujipamba na misingi ambayo Imamu na watu wa nyumbani kwake (a.s) waliipambania.
Majlisi ikafungwa kwa tenzi na qaswida za kuomboleza zilizoamsha hisia za huzuni na majonzi kutokana na yaliyojiri siku ya Ashura.
Ataba tukufu hufanya majlisi za Husseiniyya kwa lengo la kuomboleza msiba wa Ahlulbait (a.s).