Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya imefanya majlisi ya kuomboleza siku ya saba Muharam katika mkoa wa Muthannah.
Majlisi imepambwa na muhadhara kutoka kwa Shekhe Ali Abdul-Amiir, ameongea kuhusu msimamo wa Abulfadhil Abbasi (a.s) katika Ardhi ya Karbala, na mafundisho ya kudumu aliyotuachia ya kujitolea, utiifu na msimamo.
Majlisi ikahitimishwa kwa kusomwa qaswida kutoka kwa Amiri Ali Shimri, iliyoeleza msiba aliopata Imamu Hussein na watu wa nyumbani kwake (a.s).
Majlisi hiyo ni sehemu ya ratiba ya Maahadi katika kuomboleza siku hizi za Ashura na kufungamanishwa mwenendo wa Imamu Hussein (a.s) na jamii yetu.