Majlisi hiyo imehudhuriwa na kiongozi mkuu wa kisheria Muheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi, baadhi ya viongozi wa Ataba, watumishi na mazuwaru.
Majlisi imefunguliwa kwa Qur’ani tukufu, iliyosomwa na Muhammad Ridhwa Zubaidi, ukafuata muhadhara kutoka kwa Shekhe Haazim Atwawani, ameongea kuhusu safari ya Imamu Hussein (a.s) na wafuasi wake ya kwenda Karbala na ushujaa wa Abulfadhil Abbasi (a.s) katika tukio la Twafi na namna alivyo uawa kishahidi.
Majlisi ikahitimishwa kwa kusoma tenzi na qaswida za kuomboleza zilizo amsha hisia ya huzuni na majonzi kwa wahudhuriaji.
Atabatu Abbasiyya tukufu hufanya majlisi za Husseiniyya kuomboleza msiba waliopata Ahlulbait (a.s) na kuenzi mafundisho na mwenendo wao mtukufu.