Barabara za mji wa Samaraa zimejaa mawakibu za waombolezaji zikiwa na bendera zinazoashiria huzuni huku wakiimba tenzi na qaswida za uombolezaji na kuhuisha utiifu kwa Imamu mdhulumiwa.
Mawakibu za kutoa huduma mbalimbali zimejaa kwenye barabara zote zinazoelekea katika mji wa Samaraa na maeneo yanayozunguka malalo takatifu, mawakibu hizo zinagawa chakula, vinywaji na huduma zingine.









