Kamati imeratibu shindano la kitamaduni lenye anuani isemayo (Ajru-Risaalah) kwa watumishi

Kamati ya mipango katika Atabatu Abbasiyya, imeratibu shindano la kitamaduni lenye anuani isemayo (Ajru-Risaalah) kwa watumishi.

Shindano hilo linasimamiwa na kitengo cha uboreshaji na maendeleo endelevu katika Ataba tukufu, ikiwa ni sehemu ya ratiba maalum ya watumishi.

Msimamizi wa shindano hilo Dokta Hasanain Khatibu amesema “Shindano linalenga kuimarisha utamaduni na Dini kwa watumishi, sambamba na kujenga misingi bora ya maadili mema katika utoaji wa huduma”.

Akaongeza kuwa “Shindano linamaswali ya kidini na kitamaduni, yanayosaidia kuinua kiwango cha maarifa kwa washiriki”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: