Kitengo cha ujenzi kinafanya matengenezo kwenye jengo la Sayyid-Waswiyyin katika mji wa Najafu

Kitengo cha ujenzi katika Atabatu Abbasiyya kimefanya mategenezo kwenye jengo la Sayyid-Waswiyyin katika mji wa Najafu.

Miongoni mwa matengenezo hayo ni, uwekaji wa (PVC) uliofanywa na idara ya Alminiam na uwekaji wa madirisha ya kisasa katika jengo, ukarabati huo ni sehemu ya mkakati wa uboreshaji wa taasisi na majengo chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu.

Kazi imefanywa kwa kutumia vifaa vyenye ubora wa hali ya juu, kwa namna ambayo imeboresha muonekano na mazingira.

Kitengo cha ujenzi kinaendelea na utekelezaji wa miradi mbalimbali ya ujenzi katika miradi tofauti ya Ataba tukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: