Kitengo cha uboreshaji na maendeleo endelevu katika Atabatu Abbasiyya, kinafanya semina ya kimaadili kupitia program ya kupiga msasa watumishi wapya.
Semina imefanywa katika majengo ya Shekhe Kuleini chini ya Atabatu Abbasiyya, itadumu kwa muda wa siku nne.
Mkufunzi wa semina Sayyid Dhwargham Jalihawi amesema “Semina inamaudhui mbalimbali, miongoni mwake maadili ya kiislamu na umuhimu wake, misingi ya maadili mema na jinsi ya kuiimarisha pamoja na kubaini changamoto zake, kuamiliana na zuwaru na watumishi wa idara zingine, namna ya kuanzisha mfumo wa misingi ya maadili mema”.
Akaongeza kuwa “Semina imejikita katika kuanzisha mfumo wa maadili mema na kupambana na changamoto za mazingira, itahitimishwa kwa kuwapa mtihani washiriki ilikutambua namna walivyo nufaika na semina hiyo”.
Akabainisha kuwa “Semina ni sehemu ya ratiba maalum inayotekelezwa na kitengo, kwa lengo la kujenga uwezo wa watumishi wapya na kuimarisha utendaji wao kazini, ili kufikia malengo ya Atabatu Abbasiyya tukufu ya kutoa huduma bora kwa zuwaru na jamii”.




