Chuo kikuu cha Al-Ameed kimeshuhudia vikao vya shindano la Nurul-Qur’ani la kimataifa katika siku ya kwanza.
Shindano linasimamiwa na kitengo cha harakati za wanafunzi katika wizara ya elimu ya juu na tafiti za kielimu kwa msaada wa Atabatu Abbasiyya na ushiriki wa zaidi ya vyuo 60 kutoka ndani na nje ya Iraq.
Wawakilishi wa vyuo wanaoshiriki kwenye shindano hilo wamesoma Qur’ani kwa mahadhi mbalimbali, katika mazingira tulivu yanayoendana na utukufu wa kitabu cha Mwenyezi Mungu mtukufu, jambo hili linamchango mkubwa wa kujenga utamaduni wa kusoma Qur’ani kwa wanafunzi.
Kamati ya majaji inawalimu bobezi, ambao ni Dokta Basim Al-Abadi jaji wa kipengele cha hukumu za kusimama na kuanza, Shekhe Mahadi Al-Aamiry jaji wa kipengele cha ubora wa hifdhu, Shekhe Muhammad Fahami Usfuur jaji wa kipengele cha kanuni za tajwidi, Ustadh Yahaya Swahafi jaji wa kipengele cha sauti, Sayyid Hasanaini Halo jaji wa kipengele cha naghma.
Shindano hili ni sehemu ya harakati za chuo kikuu cha Al-Ameed zinazolenga kujenga misingi bora ya maadili mema kwa wanafunzi na kuwafanya waweze kushikamana na mafundisho ya Dini.













