Uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya umetangaza majina ya washindi wa shindano la waliofaulu kwenye shindano la kitamaduni katika kuadhimisha kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Bibi Zainabu (a.s).
Sharti la kupokea zawadi, anatakiwa kuja mshindi mwenyewe kwenye hafla itakayofanywa mbele ya mlango wa Qibla ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) siku ya Jumapili (4/ Jamadal-Uula/1447h) sawa na tarehe (27/10/2025m) baada ya swala ya Magharibi na Isha.
Iwapo mshindi atapata udhuru wa kushindwa kuhudhuria kwenye hafla hiyo, atatakiwa kufika kwenye ofisi za wahasibu wa Atabatu Abbasiyya tukufu ndani ya muda usiozidi wiki mbili kuanzia tarehe ya kutangazwa matokeo haya, akiwa na nyaraka zinazomthibitisha (kitambulisho cha taifa au hati ya kusafiria).
