Tukio hilo limefunguliwa kwa Qur’ani tukufu, iliyofuatiwa na usomaji wa ziara ya Abulfadhil Abbasi (a.s) kisha wimbo wa (Lahnul-Ibaa), halafu zikaimbwa qaswida na tenzi za kuomboleza zilizoeleza dhulma alizofanyiwa Bibi Fatuma Zaharaa (a.s).
Watumishi wa Atabatu Abbasiyya tukufu hufanya tukio la kiibada katika siku ya Jumatatu na Alkhamisi kila wiki.






