Miongoni mwa ratiba ya mahafali ya wahitimu.. wanafunzi wa vyuo vikuu wanafanya ibada ya kumzuru Abulfadhil Abbasi (a.s)

Wanafunzi wa vyuo vikuu vya Iraq wanaoshiriki kwenye mahafali ya wahitimu awamu ya sita, inayosimamiwa na Atabatu Abbasiyya tukufu, wanafanya ibada ya kumzuru Abulfadhil Abbasi (a.s).

Mahafali ya wahitimu wa vyuo vikuu vya Iraq (kikosi cha juu ya uongofu wa mwezi awamu ya sita), inasimamiwa na idara ya mahusiano ya vyuo na shule chini ya kitengo cha mahusiano katika Ataba tukufu, na kauli mbiu isemayo (Kutokana na wingu la Karbala umemea ukarimu), kupitia mradi wa kijana mzalendo wa Alkafeel, kwa ushiriki wa zaidi ya wanafunzi elfu 5 kutoka vyuo vikuu 75 vya serikali na binafsi katika mikoa tofauti ya Iraq.

Ibada ya ziara imefanywa na washiriki zaidi ya elfu 5 kutoka jamii tofauti, madhehebu na Dini tofauti, kisomo cha ziara kimeongozwa na Sayyid Ali Mamitha kutoka kitengo cha mahusiano katika Ataba tukufu, huku kukiwa na mazingira tulivu.

Atabatu Abbasiyya tukufu inafanya mahafali hii kwa ajili ya kuwapongeza wahitimu na kuwa mfano bora wa mahafali ya wahitimu wa vyuo vikuu, na kuhitimisha safari yao ya masomo mbele ya malalo takatifu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: