Wahudumu wa Atabatu Abbasiyya wamefanya kitendo cha kiibada ndani ya ukumbi wa haram ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), katika kuadhimisha kumbukizi ya kuzaliwa Imamu Muhammad Aljawaad (a.s).
Kitendo hicho kimehusisha usomaji wa Qur’ani tukufu, ikafuatia usomaji wa ziara ya Abulfadhil Abbasi (a.s), kisha qaswida ya (Lahnul-Ibaa), halafu zikafuata qaswida maalum kuhusu kumbukizi ya Imamu Muhammad Aljawaad (a.s) kwa ushiriki wa kundi kubwa la mazuwaru.
Wahudumu wa Atabatu Abbasiyya hufanya tukio la kiibada siku ya Jumatatu na Alkhamisi ya kila wiki.





