Kupitia maukibu ya kutoa huduma.. Idara ya Masayyid imeadhimisha kumbukizi ya kuzaliwa kiongozi wa waumini (a.s)

Wahudumu wa idara ya Masayyid katika Atabatu Abbasiyya, wameadhimisha kumbukizi ya kuzaliwa kiongozi wa waumini Imamu Ali (a.s) kwa kuhudumia zuwaru.

Wahudumu wa idara ya Masayyid wanapokea zuwaru kwa kuwapa pongezi na tabaruku, kupitia maukibu yao iliyopo mbele ya mlango wa Qibla ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) wanatoa huduma mbalimbali, kugawa maji, chai, halwa na mauwa kama sehemu ya kuadhimisha tukio hilo tukufu.

Vitengo vyote vya Atabatu Abbasiyya vinafanya kazi kubwa ya kuhudumia zuwaru wanaokuja katika mji wa Karbala kuadhimisha kumbukizi ya kuzaliwa Imamu Ali Bun Abu Twalib (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: