Kongamano la Sayyid Almujahid limeshuhudia maonyesho ya filamu inayo onyesha mwenendo wa kielimu na mradi wa kuhuisha turathi

Siku ya pili katika kongamano la kimataifa la Sayyid Almujahid imeshuhudia maonyesho ya filamu kuhusu mwenendo wake kielimu na mradi wa kuhuisha turathi.

Kongamano limeandaliwa na kituo cha Shekhe Tusi chini ya kamati kuu ya kuhuisha turathi, kwa kushirikiana na kituo cha upigaji picha nakala-kale na faharasi chini ya kitengo cha habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya, na litadumu kwa muda wa siku mbili.

Filamu imeonyesha sehemu ya maisha ya Sayyid Almujahid kielimu na kijihadi, na nasaba yake ambayo inatokana na familia kubwa kielimu, sambamba na kuonyesha vitabu muhimu alivyo andika na juhudi za kituo cha Shekhe Tusi na vituo vya Ataba tukufu katika kuhuisha turathi na kuchapisha vitabu vyake.

Filamu imesherehesha kwa ufupi kuhusu kitabu (mausua) ya (Sayyid Almujahid na turathi zake kielimu), kilicho zinduliwa siku ya kwanza ya kongamano, na kuonyesha auani za juzuu zake na majina ya waandishi.

Kongamano linalenga kuenzi kumbukizi ya Sayyid Muhammad bun Sayyid Ali bun Sayyid Muhammad Ali Twabatwabai Alhaairiy maarufu kwa jina la Sayyid Almujahid, na kueleza mwenendo wake na urithi wake katika elimu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: