Kongamano hilo limeratibiwa na kituo cha Shekhe Tusi chini ya kamati kuu ya kuhuisha turathi, kwa kushirikiana na kituo cha upigaji picha nakala-kale na faharasi chini ya kitengo cha habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya na litadumu kwa muda wa siku mbili.
Ugawaji wa zawadi umesimamiwa na makamo katibu mkuu wa Ataba tukufu Sayyid Abbasi Mussa Ahmadi, mjumbe wa kamati kuu ya Ataba tukufu Sayyid Lithi Mussawi amekabidhi zawadi kwa washiriki wa kikao cha pili, miongoni mwa waliopewa zawadi ni muongozaji mkuu wa vikao na wawasilishaji wa mada za kitafiti, kama sehemu ya kuonyesha thamani ya juhudi zao kielimu.
Kongamano linalenga kuenzi kumbukizi ya Sayyid Muhammad bun Sayyid Ali bun Sayyid Muhammad Ali Twabatwabai Alhaairiy maarufu kwa jina la Sayyid Almujahid, na kueleza mwenendo wake na urithi wake katika elimu.







