Muheshimiwa Sayyid Swafi amepongeza juhudi za Darul-Uluum Nahjulbalagha na kubariki mkakati wa harakati zake katika mwaka mpya

Kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya Muheshimiwa Sayyid Ahmadi Swali, amebariki mkakati wa harakati za mwaka mpya.

Limetokea hilo baada ya kumpokea mkuu wa Daru Dokta Meja Jenerali Atwiyya, na kusikiliza maelezo kuhusu harakati za mwaka jana na vitabu vya masomo vilivyo chapishwa na Darul-Kafeel vinavyo tegemewa kwenye selibasi ya masomo.

Muheshimiwa amepongeza juhudi za Daru na kazi kubwa iliyofanywa ya kusambaza madhumuni ya kitabu cha Nahjulbalagha, ukizingatia kuwa kitabu hicho kimefasiri na kubainisha mambo mengi yaliyomo ndani ya Qur’ani tukufu.

Muheshimiwa ameelekeza moja ya vitabu hivyo kiingizwe katika mtaala wa masomo ya shule za Al-Ameed kutokana na uzuri wa maudhui za kitabu hicho kwa wanafunzi wenye umri tofauti.

Atwiyya amesema: Katika kikao na Muheshimiwa Sayyid Swafi tumejadili mkakati wa mwaka 2026 kuhusu harakati za Daru na kazi zake, kwa lengo la kuhakikisha muendelezo wa kazi na kubaini kila jambo na malengo yake, aidha tumemuonyesha kazi tuliyofanya katika mwaka ulioisha.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: