Kitengo cha Dini kimefanya semina ya Fiqhi na Aqida kwa watumishi wa vitalu vya Alkafeel

Kitengo cha Dini katika Atabatu Abbasiyya kimefanya semina ya masomo ya Fiqhi na Aqida kwa watumishi wa vitalu vya Alkafeel chini ya Ataba tukufu.

Mkufunzi wa semina Shekhe Muhsin Asadi amesema: “Semina hii ni sehemu ya mkakati wa kitengo katika mwaka 2026, inamihadhara ya Fiqhi na Aqida katika siku ya Alkhamisi ya kila wiki”.

Akaongeza kuwa “Muhadhara wa kwanza umefafanua hukumu za udhu pamoja na kufanya kwa vitengo, kisha ratiba ikahitimishwa kwa kuswali Dhuhuraini (Adhuhuri na Alasiri) kwa jamaa”.

Kitengo cha Dini huwajengea uwezo watumishi kwenye masomo ya Fiqhi na Aqida kupitia semina hizi, jambo ambalo huwasaidia kutoa huduma bora katika vitengo tofauti vya Ataba na katika maisha yao ya kila siku.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: