Kitengo cha utalii wa kidini kimeandaa mhadhara elekezi kwa watu wanaoenda Umra kupitia msafara wa Saaqi

Kitengo cha utalii wa kidini katika Atabatu Abbasiyya, kimeandaa mhadhara elekezi kwa watu wanaenda Umra kupitia msafara wa Saaqi.

Mhadhara umetoa maelekezo ya kiidara na kusherehesha namna ya kufanya ibada ya Umra, jinsi ya kufanya Tawafu, kutia Nia, Maeneo matakatifu, Swala ya Tawafu na mengineyo miongoni mwa mambo yanayofungamana na ibada hiyo.

Msafara huondoka na muongozaji mmoja kutoka kitengo cha Dini katika Atabatu Abbasiyya, huandaa hoteli ya karibu na maeneo ya kufanyia ibada, hutoa huduma bora zinazomrahisishia mtu kufanya ibada ya Umra.

Atabatu Abbasiyya hutoa huduma bora zaidi kwa watu wanaoenda kufanya Umra kupitia msafara wa Saaqi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: