Kitengo cha habari kimehitimisha semina ya utendaji wa sauti na kudhihiri kwa habari na imewapa zawadi washiriki wa semina hiyo

Kitengo cha habari katika Atabatu Abbasiyya kimehitimisha semina ya sauti na kudhihiri kwa habari na kugawa zawadi kwa washiriki waliokamilisha vigezo na kufuzu.

Rais wa kitengo Sayyid Ali Badri amesema “Kitengo kimekamilisha semina ya sauti na kudhihiri kwa habari iliyosimamiwa na kituo cha mafunzo chini ya kitengo”.

Akaongeza kuwa “Semina imeshuhudia ugawaji wa zawadi kwa washiriki waliokamilisha vigezo na kufuzu”, akasisitiza kuwa “Kitengo kimejikita katika kuboresha uwezo wa watumishi wake na kuimarisha sekta ya habari”.

Mmoja wa washiriki wa semina, Sayyid Mustafa Ghazi amesema “Semina imeangazia namna ya kukusanya taarifa na kuzifanyia kazi” akaeleza kuwa “Siku 7 za mafunzo mfululizo zimetujenga sana, tunatarajia matokea ya mafunzo haya yataonekana katika utendaji wetu kwenye miradi ya habari ijayo”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: