Daru-Uluum Nnahjulbalagha imefanya kikao cha kujadili harakati zake za baadae

Daru-Uluum Nnahjulbalagha katika Atabatu Abbasiyya imefanya kikao cha kujadili harakati za miradi inayotarajiwa kufanywa mwaka 2026m.

Rais wa Daru Dokta Meja Jenerali Atwiyya amesema: “Daru imefanya kikao cha kujadili harakati maalum (mpango kazi) wa mwaka 2026m, kwa ajili ya kuboresha utendaji wa kazi zake kwa namna ambayo inaendana na malengo ya Ataba tukufu”.

Akaongeza kuwa “Kikao kimejadili mpango kazi na mafanikio yaliyopatikana katika mwaka 2025, maelekezo ya kiutawala kutoka Ataba tukufu sambamba na kuangazia mkakati wa mwaka mpya na kusikiliza maoni ya watumishi wa Daru na mapendekezo yao”.

Daru-Uluum Nnahjulbalagha ni kituo cha kielimu kinachosambaza fikra za Imamu Ali (a.s) kupitia program za utafiti zinazosaidia kujenga uelewa wa kibinaadamu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: