Kitengo cha mgahawa katika Atabatu Abbasiyya kimepokea wahitimu wa chuo cha Jeshi chini ya wizara ya ulinzi ya Iraq kikosi cha 89 waliokuja kutabaruku kwa kupata chakula cha mchana.
Wahitimu wamesoma kiapo cha kuhitimu mbele ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), ikafuatiwa na ibada ya ziara.
Maelfu ya wahitimu wa chuo cha Jeshi na vyuo vikuu vingine vya Iraq, husoma kiapo cha utii katika Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya.





