Muheshimiwa Sayyid Swafi amesisitiza umuhimu wa mafunzo mfululizo ya kujenga uwezo wa wahudumu wa afya na kuboresha huduma.

Kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya Muheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi, amesisitiza umuhimu wa mafunzo mfululizo ya kujenga uwezo wa wahudumu wa afya na kuboresha huduma.

Hilo limetokea wakati Muheshimiwa alipompokea rais wa kitengo cha madaktari Dokta Haifa Tamimi, na akasikiliza maelezo ya program za kitengo na mikakati yao, ikiwemo program ya mafunzo kwa watumishi wake kwa kushirikiana na hospitali ya rufaa Alkafeel, pamoja na kuongea kuhusu ufunguzi wa kituo cha Jafari Alhilliy cha huduma za dharura kwa zuwaru.

Muheshimiwa akausia umuhimu wa mafunzo ya kuwajengea uwezo watumishi wa kitengo, kikiwemo kituo cha Alhiliy kitakacho zinduliwa hivi karibuni, sawasawa wawe watumishi wa kawaida, wauguzi na madaktari.

Akasisitiza kuwa semina huchangia kujenga uwezo wa watumishi na kuboresha huduma.

Dokta Haifa Tamimi akasema: “Hakika kikao na Muheshimiwa Sayyid Swafi, kumekuwa na mazungumzo yaliyojikita katika kueleza umuhimu wa semina endelevu, na kipindi cha ufunguzi wa kituo cha Jafari Alhiliy, tumepata Baraka za Muheshimiwa kuhusu ufunguzi wa kituo hicho siku zijazo”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: