Majlisi ya kuomboleza imefanywa ndani ya ukumbi wa malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), imehudhuriwa na kundi kubwa la zuwaru na itaendelea kwa muda wa siku tatu, asubuhi na jioni.
Mhadhiri wa majlisi katika kipindi cha asubuhi kuanzia siku ya kwanza Shekhe Haazim At-wani, amekuwa akiongea maudhui tofauti, ikiwa ni pamoja na magumu aliyopitia Imamu Mussa bun Jafari (a.s) wakati alipokuwa anahamishwa jela moja hadi nyingine.
Ameongea kuhusu mazingira magumu aliyopitia (a.s) kutokana na msimamo wake mbele ya watu waovu, akataja msimamo yake na mwenendo wake mtukufu.
Atabatu Abbasiyya huadhimisha matukio yanayohusu Ahlulbait (a.s), kwa lengo la kueleza historia yao na mwenendo wao mtukufu.



