Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya imeweka vituo vya usomaji wa Qur’ani katika barabara zinazotumiwa na zuwaru wanaoenda katika mji wa Kadhimiyya jijini Baghdad, kuomboleza kumbukizi ya kifo cha Imamu Mussa Alkadhim (a.s).
Maahadi ya Qur’ani tukufu katika mji wa Najafu chini ya Majmaa-Ilmi imeweka kituo cha usomaji wa Qur’ani katika kitongoji cha Dabuni kaskazini ya mkoa wa Waasit, ikiwa ni sehemu ya program ya Qur’ani inayolenga kuhudumia zuwaru na kuwapa maelekezo ya kidini wakati wa safari yao.
Kituo kimejikita katika kufundisha usomaji sahihi wa surat Fat-hah, kutokana na umuhimu wake katika swala, sambamba na kujenga uelewa kuhusu Qur’ani na kusambaza utamaduni wa kusoma kitabu cha Mwenyezi Mungu mtukufu baina ya zuwaru.
Program ya kuweka vituo vya usomaji wa Qur’ani katika barabara zinazotumiwa na zuwaru wa Rajabiyya inafanywa kwa mwaka wa tano mfululizo kwenye kitongoji cha Dabuni, vituo vinapata muitikio mkubwa kutoka kwa mawakibu Husseiniyya na zuwaru.




