Atabatu Abbasiyya tukufu inaendelea kufanya majlisi za kuomboleza kifo cha Imamu Alkadhim (a.s) katika ukumbi wa haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s).
Majlisi imeandaliwa na idara ya wahadhiri wa Husseiniyya chini ya Ataba tumufu, asubuhi na jioni, itaendelea kwa muda wa siku tatu.
Mhadhiri wa majlisi Shekhe Jaasim Alhaatimi katika siku ya kwanza, ameongea kuhusu historia ya Imamu Mussa bun Jafari (a.s), elimu na utukufu wake, akaeleza mazingira magumu aliyoishi ndani ya jela za madhalim kwa ajili ya kunusuru Dini na kulinda sheria za kiislamu.
Atabatu Abbasiyya tukufu huadhimisha matukio yanayohusu Ahlulbait (a.s), kwa lengo la kujenga uwelewa wa historia yao na kufuata mwenendo wao mtukufu.



