Wahitimu wa chuo cha polisi nchini Iraq kikosi cha 70 wamesoma kiapo cha kuhitimu mbele ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s).
Atabatu Abbasiyya imepokea makundi ya maofisa wa polisi ya Iraq kikosi cha 70 kutoka mikoa tofauti ya Iraq, wamesoma kiapo cha utiifu kwa taifa mbele ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s).
Usomaji wa kiapo umehudhuriwa na wazazi wa wanafunzi wanaohitimu na kundi kubwa la zuwaru, jambo hili limekuwa utamaduni wa wahitimu wa vyuo na Maahadi hapa Iraq.
Maelfu ya wanafunzi wanaohitimu vyuo vikuu vya Iraq na vyuo vya kiaskari kila mwaka, husoma kiapo cha kuhitimu mbele ya malalo ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s).





