Rais wa ujumbe wa Ataba tukufu Sayyid Khalili Mahadi Hanun amesema “Maukibu ya Ataba tukufu hutoa huduma mbalimbali kwa zuwaru wa Imamu Mussa bun Jafari Alkadhim kila mwaka wakati wa kuomboleza kifo chake”.
Akaongeza kuwa “Maukibu inatoa huduma kupitia vituo viwili, cha kwanza katika barabara ya Swahibu Zamaan (a.f), kingine katika barabara ya Bubu-Muraad, tunaendelea kuongea na Atabatu Kaadhimiyya tukufu kwa ajili ya kuangalia uwezekano wa kufungua vituo vingine vya maukibu sambamba na kuongezeka idadi ya zuwaru”.
Akabainisha kuwa “Milo mitatu ya chakula inatolewa kila siku kwa zuwaru, pamoja na chakula chepesi” akasema “Vitengo vingi vya Ataba tukufu vinashiriki katika kutoa huduma mbalimbali”.
Akafafanua kuwa “Kitengo cha magari kinafanya kazi ya kubeba zuwaru kuwatoa na kuwapeleka katika malalo takatifu, huku kitengo cha utumishi kikisaidia kuondoa taka kwa kutumia gari zake za kubeba taka, hali kadhalika kitengo cha afya kimeandaa kituo cha kutoa huduma za matibabu kwa zuwaru na kitengo cha kulinda nidham kinasaidia kusimamia matembezi ya waombolezaji”.








