Muheshimiwa Sayyid Swafi amesisitiza umuhimu wa kuandaa orodha ya mahitaji ya vituo vya Atabatu Abbasiyya vya nje

Kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya Muheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi, amesisitiza umuhimu wa kuandaa orodha ya mahitaji ya vituo vya Atabatu Abbasiyya vya nje.

Ameyasema hayo alipompokea msimamizi wa kitengo cha nje Sayyid Jawadi Hasanawi na rais wa kitengo Sayyid Swadiq Laazim, na kusikiliza maelezo ya kina kuhusu huduma zinazotolewa na kitengo.

Muheshimiwa amesisitiza umuhimu wa kuandaa orodha ya mahitaji ya vituo vya nje, kwa lengo la kurahisisha ufuatiliaji wa kila kinachohitajika.

Akaeleza umuhimu wa kuwa kitengo ndio msaidizi wa vituo na sio mbadala wake.

Kwa upande wake Sayyid Swadiq Laazim amesema, kikao na Sayyid Swafi kimetupa nafasi ya kuonyesha harakati zinazofanywa na kitengo, huduma zinazotolewa, hususan baada ya upanuzi wake, sambamba na kueleza changamoto zilizopo katika vituo vya nje na kuangazia utatuzi wa changamoto hizo katika utoaji wa huduma.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: