Atabatu Abbasiyya imefanya majlisi ya kuomboleza kumbukizi ya kifo cha Imamu Alkadhim (a.s) karibu na malalo yake takatifu

Ujumbe wa Atabatu Abbasiyya umefanya majlisi ya kuomboleza kifo cha Imamu Alkadhim (a.s) karibu na malalo yake takatifi katika mji wa Kadhimiyya jijini Baghdad.

Rais wa ujumbe huo Sayyid Khalili Mahadi Hanun amesema “Majlisi imefanywa katika maukibu ya Ataba tukufu, karibu na malalo ya Imamu Mussa Alkadhim (a.s) wakati wa kuomboleza kumbukizi ya kifo chake”.

Akaongeza kuwa “Mhadhiri wa majlisi hiyo alikuwa ni Sayyid Akram Mussawi, ameeleza historia ya Imamu Mussa Alkadhim (a.s) na dhulma aliyofanyiwa wakati wa uhai wake”.

Atabatu Abbasiyya tukufu inatoa huduma mbalimbali katika mji wa Kadhimiyya wakati huu wa kuomboleza kifo cha Imamu Alkadhim (a.s), miongoni mwa huduma hizo ni: ugawaji wa chakula, huduma za afya na huduma zingine kwa kushirikiana na kamati maalum za mji huo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: