Kitengo cha utalii wa kidini kinafanya msafara wa Saaqi wa ibada ya Umra

Kitengo cha utalii wa kidini katika Atabatu Abbasiyya kinafanya msafara wa Saaqi wa ibada ya Umra.

Kiongozi wa idara ya misafara ya nje katika kitengo hicho Sayyid Abdullahi Karim amesema “Kitengo kinafanya msafara wa Saaqi kwa njia ya anga, kuanzia uwanja wa ndege wa Najafu hadi katika mji mtakatifu wa Maka”.

Akaongeza kuwa “Msafara unaongozwa na watumishi wa kitengo na muelekezaji wa mambo ya kidini kutoka kitengo cha Dini katika Atabatu Abbasiyya tukufu, msafara wetu huandaa hoteli za karibu na maeneo ya kufanyia ibada ya Umra ili kuondoa usumbufu wakati wa utekelezaji wa ibada hiyo”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: