Uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya, umefanya majlisi ya kuomboleza kumbukizi ya kifo cha Imamu Mussa bun Jafari Alkadhim (a.s) ndani ya ukumbi wa utawala.
Mhadhiri wa majlisi, Sayyid Ahmadi Yaqobo amesema: “Tumefanya majlisi ya kuomboleza kifo cha Imamu Alkadhim (a.s), katika siku hizi tunajikumbusha historia yake takatifu”.
Akaongeza kuwa “Katika majlisi hii tumeeleza historia ya Imamu Alkadhim (a.s), elimu yake, utukufu wake na namna ya ulinganiaji wake”.
Atabatu Abbasiyya huadhimisha matukio yanayohusu Ahlulbait (a.s) na kueleza utukufu wao na mwenendo wao.




