Kitengo cha maelekezo ya kisaikolojia na malezi katika chuo kikuu cha Alkafeel, kimefanya majlisi ya kuomboleza kifo cha Imamu Alkadhim (a.s).
Majlisi imehudhuriwa na rais wa chuo Dokta Nuris Dahani na msaidizi wake Dokta Nawaal Almayali, wakuu wa vitivo na wasaidizi wao na idadi kubwa ya watumishi wa chuo.
Majlisi imefunguliwa kwa Qur’ani tukufu iliyosomwa na Sayyid Muhandi Almayali, ukafuata muhadhara wa kidini kutoka kwa Shekhe Jafari Alwaaili, ameeleza sehemu ya maisha ya Imamu Mussa Alkadhim (a.s), akasisitiza umuhimu wa kufuata mwenendo wake ili kuimarisha maelewano na uadilifu katika jamii.





