Kumbukumbu ya kifo chake inasadifu siku ya mwezi ishirini na tano Rajabu, idadi kubwa ya waumini imeingia katika mji wa Kadhimiyya, kukiwa na mawakibu nyingi za utoaji wa huduma mbalimbali kwa waombolezaji.
Atabatu Abbasiyya tukufu inatoa huduma kupitia maukibu mbili, moja ipo karibu na malalo takatifu, inagawa maelfu ya sahani za chakula.
Ataba inasaidia kutoa huduma zingine pia, kama vile kuongoza matembezi ya waombolezaji, kutoa huduma za matibabu, usomaji wa Qur’ani na kujibu maswali ya kifiqhi kutoka kwa zuwaru.





